Header Ads

NIKKI WA PILI AMPIGIA SALUTI R.O.M.A


Nikki wa Pili.
STAA wa muziki wa Hip Hop Bongo, Nickson Simon ‘Nikki wa Pili’ amempigia saluti msanii mwenzake, Ibrahimu Musa ‘R.O.M.A Mkatoliki’ kwa kusema anamkubali kwa kuwa hajawahi kumuangusha kwenye uandishi wa ngoma zake kali za kiharakati.

Akichonga na Mikito Nusunusu Nikki alisema, amekuwa shabiki wa nyimbo za R.O.M.A ambazo ni za kiharakati kwa muda mrefu na hajawahi kumuangusha hata mara moja kwenye utunzi na maudhui ya ngoma zake ikiwemo hii mpya ya Zimbabwe.
R.O.M.A.
“Licha ya kuwa nami ni mwanamuziki wa Hip Hop lakini namkubali sana R.O.M.A maana kila ngoma anayotoa ni kali, hata huu wimbo wake wa Zimbabwe umenisababisha niendelee kumwona katika jicho pana zaidi, naziona tuzo kadhaa kwa rapa huyo, ukweli ni kwamba anajua kutunga, anajua kuyachezea maneno vile anavyotaka, kweli jamaa anatisha sana,” alisema Nikki.

No comments