NAY WA MITEGO AFUNGUKIA BIFU LAKE NA ROMA
HIT MAKER wa ngoma inayobamba kwa sasa Acheze, Emmanuel Elibariki ‘Nay Wa Mitego’, amesema aliumizwa sana na maneno ya rapa mwenziye, Roma Mkatoliki, aliyeongea maneno ya kumkashifu mara baada ya kuibuka baada ya kutekwa kwake, miezi michache iliyopita.
NAY WA MITEGO AFUNGUKA…
“Roma anatakiwa ajue kwamba mimi ni mmoja kati ya wasanii ambao walishinda kutwa nzima kwenye studio yake ya Tongwe Records na kituo cha polisi, toka siku aliyotekwa hadi siku aliyopatikana, lengo likiwa ni kutaka kujua tunasaidiana vipi ili aweze kupatikana.
“Akitaka kuthibitisha hilo amuulize mkewe, lakini nikashangaa baada ya kupatikana eti akanikashifu, kila nikikumbuka inaniumiza, sema mimi ni mwanaume siweki vitu rohoni, na pia nimeipenda sana ngoma yake ya Zimbabwe, Roma ni rapa mkali, sina kipingamizi juu ya hilo,” amesema Nay Wa Mitego.
Post a Comment