Mtangazaji Dida Afunguka Kuhusu Kuolewa Tena Baada ya Ndoa zake Tatu Kubuma.......
MTANGAZAJI wa Radio Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’ ambaye hadi sasa anashikilia rekodi yake ya kufunga ndoa mara tatu kisha kuvunjika, amefunguka kuwa kwa sasa hawezi kukurupuka kuolewa kama ilivyokuwa kwa ndoa za mwanzo ndiyo maana amekaa kwenye uchumba kwa muda mrefu.
Dida ambaye miezi kadhaa iliyopita alivishwa pete ya uchumba na Mwenyekiti wa Kijiji cha Ukuni, Bagamoyo, Issa Seleman aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, hawezi kukurupuka kuingia kwenye ndoa kama zile za mwanzo kwani ana nia njema na ni kitu cha neema hivyo haihitaji kuwa na haraka.
“Siwezi kukurupuka tena kama ndoa za mwanzo, sina haraka kwa sasa, kuna vitu vinakamilishwa kwanza ndiyo maana uchumba wa muda mrefu,” alisema Dida.
Stori: Gladness Mallya, Dar

Post a Comment