Mimi na Ben Pol sasa hivi tunafanya vitu vya ndani – Ebitoke
Mchekeshaji Ebitoke amedai si kweli penzi lake na Ben Pol limekufa bali wanafanya mambo yao kwa usiri zaidi.
“Mimi na Ben Pol sasa hivi tunafanya vitu vya ndani kwa ndani, hatutaki tuviweke hadharani. Hamna siyo vya unyago na siwezi kumuongelea vibaya Bentoke labda watu wanaona haniposti mimi kila siku lakini si hivyo,” ameiambia Times Fm.
Mchekeshaji huyo amesema mipango walionayo kwa sasa ndio inapelekea kutoonekana pamoja kwa sasa na kupostiana kwenye mitandao ya kijamii.
“Tunamipango mingi, kwanza kufanya kazi pamoja na kushirikiana katika jambo lolote na ameniaidi lazima ahakikishe natimiza malengo yangu na ameona mimi bado ni mdogo ananifundisha kila kitu jinsi gani nikue kwenye hii tasnia na the way hii mitandao ya kijamii ilivyo na maneno ya watu yalivyo,” amesema.
Couple ya wasanii hawa imekuwa ikichukuliwa kama kiki kitu kilichochangiwa na uvumi kuwa mmoja wapo alilipwa ili kufanikisha hilo kitu ambacho wote wamekuwa wakikana.
Post a Comment