Header Ads

MECHI ZA KIRAFIKI NA WAGANDA, KOCHA AZAM FC AONA MWANGA KIKOSINI MWAKE



Kocha Mkuu wa Azam, Mromania, Aristica Cioaba, amefunguka kuwa kambi ya kikosi hicho ya nchini Uganda imemwezesha kupata kikosi cha kwanza ambacho atakitumia kwenye mechi mbalimbali za Ligi Kuu Bara.

Azam ilikwenda nchini Uganda kuweka kambi ya wiki mbili ya kujiweka sawa kabla ya kuanza kwa mikikimikiki ya ligi kuu, ambapo wakiwa huko walicheza mechi kadhaa za kirafiki na timu za URA, KCCA na Vipers.

Mromania huyo amesema kuwa kambi hiyo imekuwa na faida kwake kutokana na kuwatumia wachezaji wote jambo ambalo limemsaidia kupata kikosi chake cha kwanza.

“Kambi yetu ya Uganda imekuwa na faida sana kwetu kwa sababu niliwatumia wachezaji wote ambao tulienda nao huko na jambao hilo limenisaidia kupata wale ambao nitakuwa nawaanzisha kwenye kikosi cha kwanza.


“Naamini hao niliwachagua watatoa upinzani mkubwa kwa wapinzani wetu, lakini hata hao ambao wamekosa nafasi kwenye kikosi hicho cha kwanza wana viwango vikubwa ambavyo vitatusaidia kufanya vizuri kwenye makombe ambayo tunashiriki,”alisema Mromania huyo.

SOURCE: CHAMPIONI

No comments