MASHABIKI SIMBA WAINGIA HOFU KUHUSIANA NA KIKOSI CHAO KUJIAMINI SANA
Mashabiki wa Simba wamewaonyesha wachezaji wao kuacha kujiamini kupindukia kwa kuwa inaweza kuchangia kupoteza mechi dhidi ya Yanga.
Simba inajiandaa kuivaa Yanga katika mechi ya Ngao ya Jamii kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, wikiendi hii.
Lakini mashabiki hao waliotuma maoni yao kupitia mtandao wa Blog ya Hamisihemedi na mitandoa ya kijamii ya hamisihemedi wamesema, wachezaji wao wameonyesha kujiamini kupindukia ambalo ni jambo baya sana.
Wengi wamewataka wachezaji kucheza kwa juhudi badala ya kuamini wao ni nyota.
BAADHI YA WALIOANDIKA UJUMBE WAO:
“Kweli usajili ni mzuri lakini lazima wachezaji wajue kwamba kujituma ni muhimu na mpira hautaki dharau,” aliandika Mohammed Mwakisu wa Mbezi Tangi Bovu, Dar.
“Naona Simba wamesajili vizuri lakini wanaweza kupotea kwa kuwa wanajiamini sana,” aliandika Henry Jambo wa Kigoma.
“Nina hofu sana kuwa Simba watafungwa, naona wachezaji wake wanajiamini kupindukia. Wacheze mpira sio kuonyesha wao ni maarufu,” aliandika Joseph Minde wa Shinyanga.
Post a Comment