Header Ads

FAIZA: MNIACHE NI LIFE STYLE YANGU


FAIZA
Mwanadada asiyeishiwa vituko, ‘Faiza’ katika pozi matata
MUIGIZAJI anayejipatia umaarufu kutokana na vituko, Faiza Ally amewataka watu wanaomkosoa kuachana naye kwa vile hayo ndiyo aina ya maisha aliyoamua kuishi (life style).

Alitoa kauli hiyo kufuatia watu mbalimbali kumkosoa kwa kitendo chake cha kuonekana akiwa mitaani na mtoto wake aliyezaliwa hivi karibuni, huku wakosoaji wakisema ilikuwa ni mapema mno kumtembeza mitaani hasa kwa kuwa hata siku 40 hajafikisha tangu azaliwe.

“Unajua kila mtu ana life style yake, haya ni maisha yangu niliyochagua na mambo yanabadilika, naishi kuendana na wakati, kwa hiyo nawashauri watu waache kukariri, siyo lazima watu wote tufanane,” alisema.

NA: GLADNESS MALLYA| RISASI

No comments