Diego Costa amponda Antonio Conte huku akimmwagia sifa Jose Mourinho
Diego Costa anakaribia kupata klabu mpya, unaonekana Costa hakutaka kuondoka Chelsea lakini ugomvi wake na kocha Antonio Conte umechangia kwa kiasi kikubwa mshambuliaji huyo kuamua kuondoka.
Sasa baasi Diego Costa ameulizwa kuhusu kocha huyo wa Chelsea na bila kufikiria mara mbili Costa amesema Conte ni kocha mzuri lakini ni kocha ambaye hawezi kuishi vizuri na wachezaji wake.
“Unajua mwezi wa kwanza nilikuwa nataka kuongeza mkataba lakini kuna mambo.yalitokea na sikufanya hivyo na najua kocha alikuwa chanzo cha mimi kutofanya vile” alisema Costa.
“Namuheshimu sana ni kocha ambaye amefanya mambo makubwa lakini linaookuja suala la utu hapana kwani hajui kuishi na wachezaji na anakuwa mbali nao sana”
Wakati Costa akimshushia shutuma hizo Conte ,Diego huyo huyo amemwagia sifa kocha wa Manchester United Jose Mourinho baada ya kocha huyo kumpigia simu.
“Mourinho alinipigia simu moja kwa moja akiniuliza kama nina matatizo na kutaka kujua naendeleaje baadae alinitakia kila la kheri, ni mtu ambae nina uhusiano nae mzuri na kila mmoja wetu alihuzunika alipoondoka” alisema Costa.
Post a Comment