Header Ads

BREAKING NEWS: MSUVA, CHIRWA, KASEKE WATOLEWA TAMKO NA KAMATI YA NIDHAMU TFF


Msuva akimfuata mwamuzi.
KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imemkuta na makosa ya utovu wa nidhamu aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga anayekipiga nchini Morocco, Simon Msuva ambaye imempa onyo kali la barua.
Msuva, Obrey Chirwa na Deus Kaseke walijadiliwa na kamati hiyo kwa utovu wa nidhamu ambapo walikuwa wakituhumiwa kumsukuma mwamuzi kwenye mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Yanga SC na Mbao FC ya Mwanza.
Aidha TFF imewasamehe Chirwa na Kaseke baada ya kutowakuta na hatia katika sakata hilo.
Msuva ametua leo nchini ambapo ataungana na wenzake kuitumikia Taifa Stars kwenye mechi na Timu ya Taifa ya Botswana.

No comments