Header Ads

Baada ya vita ya Morata, Madrid wazirudisha tena ulingoni Chelsea na United


Alvaro Morata alikuwa mchezaji ambaye alizifanya Manchester United na Chelsea kuvutana sana kuhusu usajili wake, baadae Morata aliamua kujiunga na Chelsea huku United wakimnunua Lukaku.
Sasa Chelsea na Manchester United zinaweza kuingia upya vitani katika usajili mwingine, na safari hii pia kama ilivyokuwa mwanzo mchezaji atakayegombaniwa na Chelsea na United anatokea Real Madrid.
Ni Gareth Bale, mustakabali wa Gareth Bale ndani ya klabu ya Real Madrid sio mzuri na kama Madrid wakafanikiwa kumnunua Kylian Mbappe kama inavyosemekana, baasi ni wazi kwamba nafasi ya Bale ndani ya Madrid itakuwa ngumu sana.
Manchester United kwa muda sasa wamekuwa wakipambana kutafuta saini ya Gareth Bale na inasemekana matajiri wa United walikuwa tayari kutuma ofa ya £90m kwa Madrid ili kumnasa Gareth Bale.
Chelsea nao wameamua kufuatilia hali inayoendelea kati ya Bale na Madrid, na ikumbukwe kwamba hata kabla hajatua Real Madrid, klabu ya Chelsea walishawahi kujaribu kumnunua toka Tottenham.
Klabu hizo zote mbili zinamhitaji sana Bale kwani United wanamuona kama mtu sahihi baada ya kumkosa Perisic na vilevile Chelsea nao wanahitaji mtu wa kucheza upande wao wa kushoto huku pia wakitafuta mtu wa kukaa nafasi ya Eden Hazard kama akiondoka.

No comments