Header Ads

Alvaro Morata amkimbia Harry Kane


Alvaro Morata ameshasaini Chelsea na sasa ni mchezaji rasmi wa klabu hiyo huku tayari ameshaitumikia katika michezo miwili iliyopita na wakipoteza yote.
Wakati Morata akiwa Hispania kulikuwa na tetesi nyingi juu ya uhamisho wake kutoka Real Madrid kwenda EPL na timy nyingi zilionekana kutaka saini ya mshambuliaji huyo.
Moja ya klabu ambayo ilikuwa inataka kumnunua Morata ilikuwa ni Tottenham Hotspur na kocha wa timu hiyo Maurcio Pochettino alishawahi kuzungumza na Morata mwaka jana.
Pochettino alikuwa akimshawishi Morata kujiunga na Tottenham lakini hofu kubwa ya Morata ilikuwa uwepo wa Harry Kane katika klabu ya Tottenham.
“Siku moja aliniuliza, kwanini unisajili mimi wakati una Kane au unataka nikae katika benchi?” alisema Pochettino, Morata alikuwa akitaka nafasi lakini ilikuwa ngumu kucheza mbele ya Kane.
Baadaye ndipo Morata aliona ni bora aende Chelsea ambako Diego Costa anaelekea kuondoka na hivyo inaweza kumpa nafasi ya kupata namba tofauti na Tottenham alipo Harry Kane.

No comments