Header Ads

Yanga imemsajili golikipa mcameroon


Klabu ya Yanga imemsainisha mkataba wa miaka miwili golikipa wa African Lyon Youthe Rostand ambaye ni raia wa Cameroon aliyefanya vizuri msimu uliopita licha ya klabu yake kushuka daraja.
Yanga wamesajili Rostand huku kukiwa na tetesi kwamba golikipa wa Yanga Deogratius Munishi ‘Dida’ kwamba ametimkia Afrika Kusini kufanya majaribio lakini hadi sasa bado haijafahamika ni kwenye klabu gani.
Rostand anaingia Yanga kusaidiana na Beno Kakolanya huku Ally Mustafa akitajwa kuondoka kwenye kikosi hicho cha Jangwani na amekuwa akihusishwa kujiunga na Singida United.

No comments