Header Ads

Viwango vipya vya Uefa,Diego Simeone azivua nguo klabu za Epl,Barca na Bayern


Klabu ya soka ya nchini Hispania ya Atletico Madrid imeipita miamba mikubwa ya soka ya Ulaya kama Barcelona na Real Madrid katika orodha mpya iliyotangazwa na shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA).
Katika orodha ya vilabu bora barani Ulaya klabu bingwa Ulaya Real Madrid wanaongoza orodha hiyo wakiwa na wastani wa kura 151.799 wakifuatiwa na majirani zao wa mji wa Madrid klabu ya Atletico yenye 133.799.
Haya ni mafanikio makubwa sana kwa kocha wa klabu hiyo Diego Simeone kwani mwaka 2011/2012 wakati akiichukua Atletico ilikuwa katika nafasi ya 23 katika viwango hivyo na hii inamaanisha ameipandisha kwa viwango 21 juu zaidi.
Katika misimu minne iliyopita klabu hiyo ya Atletico Madrid imeshiriki fainali za Champions League mara mbili lakini kama hiyo haitoshi katika msimu unao wa Champions League kocha Diego Simeone ataweka rekodi ya kuipeleka Atletico katika mashindano hayo mara 5 mfululizo.
Wakati kocha Diego Simeone akianza kuifundisha Atletico, Manchester United walikuwa nafasi ya pili,Chelsea ya tatu,Arsenal ya sita na Liverpool ilikuwa ikishikilia nafasi ya 11 katika msimamo huo lakini sasa mambo yamebadilika.
Kwa sasa Arsenal ni ya 11,Chelsea ya 13,Manchester United ya 16,Liverpool ya 35 huku timu inayoongoza katika msimamo huo kutoka Epl ikiwa ni Manchester City walioko nafasi ya 9 katika msimamo huo.
Klabu ya Barcelona wako katika nafasi ya tatu ya msimamo huo wakiwa na wastani wa kura (128.7), Bayern wakiwa nafasi ya nne (122.65) huku mabingwa wa ligi kuu nchini Italia ya Serie A klabu ya Juventus wakiwa nafasi ya tano (119.04).

No comments