Header Ads

United wawang’ang’ania Lukaku na Morata


Jana kulikuwa na taarifa kutoka kwamba kocha Jose Mourinho hana furaha na jinsi dirisha la usajili linavyoendelea katika klabu hiyo na anaona usajili huo unaenda taratibu sana tofauti na alivyotaka.
Lakini sasa klabu hiyo inaonekana imesikia masikitiko ya Mourinho na wameamua kulivalia njuga suala la usajili huku bado majina ya nyota wawili wakubwa Alvaro Morata na Romelu Lukaku yakizungumziwa.
Jarida moja la michezo nchini Hispania limetoa taarifa kwamba yamebaki masaa tu ili usajili wa mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata kwenda katika klabu ya Manchester United ukamilike.
Marca linasema pande zote mbili yaani Manchester United na Real Madrid wameshakubaliana kuhusu uhamisho wa nyota huyo lakini kilichobaki ni masuala ya sahihi tu ambayo yanaweza kukamilika katika wiki hii.
Lakini wakati United wakitajwa kumalizana na Morata, mchezaji mwingine anayehitajika Old Traford ni Romelu Lukaku na siku za karibuni anaonekana yuko busy akila bata nchini Marekani akiwa na Paul Pogba.
Kuhusu Lukaku taarifa zinasema sasa Manchester United wameamua kufanya kweli kumnunua nyota huyo baada ya Chelsea walioonekana kumtaka kuonekana kuanza kushindwa kumnunua.
United wanajipanga pia kumtoa Rooney kwenda Everton kama chambo ya kumnunua Lukaku ambaye thamani yake inatajwa kuwa ni €100m, kama Rooney akienda Everton baasi anaweza kuja na timu ya Everton nchini Tanzania siku ya tarehe 13.

No comments