Header Ads

Tetesi za usajili Ulaya, Rooney kuja Bongo?


Siku zinazidi kuhesabika kwa safari ya Everton kuja nchini Tanzania,lakini tetesi mpya kutoka ndani ya klabu hiyo ni usajili wa Wayne Rooney ambapo inasemekana mshambuliaji huyo anaweza kusaini katika klabu ya Everto .
Klabu ya soka ya Real Madrid imekamilisha usajili wa Theo Hernandez kutoka katika klabu ya Atletico Madrid ambapo dau la €24m ambapo amesaini mkataba wa miaka 6.
Baada ya kimsaini mshambuliaji wa Olympique Lyon Alexandre Lacazette, sasa klabu ya Arsenal imepiga hodi katika klabu ya Monaco kwa ajili ya kumnunua mlinzi Thomas Lemar.
Inasemekana kocha wa Manchester United Jose Mourinho hana furaha na jinsi klabu hiyo inavyoendesha suala la usajili, Mourinho anawataka wachezaji kadhaa wakubwa lakini inaonekana kuchelewa.
Baada ya kupoteza namba ya kudumu katika kikosi cha Real Madrid hatimaye mlinzi wa kushoto wa klabu hiyo Fabio Contrao amesaini kuichezea klabu ya Sporting CP kwa mkopo.
Taarifa zinasema vilabu vya Chelsea na As Roma  vimeshafanya makubaliano kuhusu uhamisho wa beki Antonio Rudiger ambapo atakwenda Chelsea kwa dau la €34m.

No comments