Header Ads

Tetesi za usajili barani Ulaya


Baada ya beki Alexandre Kolarov kuomba kuondoka Man City sasa boss wa timu hiyo Pep Gurdiola amejipanga kurudi tena sokoni kununua mabeki watatu kwa ajili ya kukosi chake msimu ujao.
Inasemekana klabu ya Barcelona umeanza kumfuatilia Philippe Coutinho lakinj klabu ya Liverpool imekataa ofa yao ya £72m na kusisitiza kwamba kiungo huyo hauzwi kwa dau lolote kwa sasa.
Klabu ya Everton imejioanga kumnunua mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud baada ya klabu ya Dortmund ambao nao walikuwa wakimtaka Giroud kuamua kuachana na mchezaji huyo.
Tetesi za Neymar kwenda PSG zimezidi kushika kasi na sasa taarifa zinasema karibia 95% ya suala hilo la usajili imeshakamilika na siku sio nyingi Neymar atatua PSG.
Zlatan Ibrahimovich ataamua hatma yake kama ataendelea na United au hapana kutokana na mwenendo wa timu hiyo, inasemekana kwa sasa Zlatan anafuatilia kwa karibu maendeleo ya timu hiyo kabla ya kufanya maamuzi.
Shirika moja kubwa la habari nchini Uingereza limesema lina uhakika Man City ndio klabu iliyofanya mazungumzo ya siri na Kylian Mbape na sasa Monaco wanajipanga kwenda kuishtaki klabu hiyo na nyingine zilizofanya hivyo.
Baada ya kumpoteza Mohamed Salah sasa klabu ya As Roma inataka kumnunua Ryad Mahrez ambaye wanamuona kama chaguo namba moja katika kuziba pengo la Salah.

No comments