Header Ads

Tetesi za usajili barani Ulaya wikiendi hii


Baada ya ukimya wa muda mrefu hatimaye Alexis Sanchez amevunja ukimya kwa kusema anataka kucheza michuano ya Champions Leaugue msimu ujao, hii inamaanisha anaweza kuondoka Arsenal kwani hawapo katika mashindano hayo.
Katika kuonesha jeuri waliyonayo, klabu ya Manchester United inaamini kwamba sio Real Madrid tu lakini kwa sasa hakuna klabu yenye uwezo wa kumnunua mlinda lango wao David De Gea.
Baada ya ofa yao ya £ 57m kukataliwa, klabu ya Liverpool bado haijakata tamaa na imejipanga kurudi tena kwa ajili ya kumsajili kiungo wa klabu ya Rb Leipzig ya nchini Ujerumani Nabby Keita.
Taarifa zinasema baada ya klabu ya Chelsea kumnunua Timoue Bakayoko kutoka Monaco sasa wanajaribu kumshawishi Gonzalo Higuain ajiunge nao ambapo dau lao la kwanza kumnunua mshambuliaji huyo limekataliwa na Juventus.
Klabu ya Ac Milan inaendelea kufanya fujo kubwa katika dirisha hili la usajili,tayari wiki hii Leornardo Bonucci alimwaga wino kuitumikia klabu hiyo na sasa mashambulizi yamegeuka kwa kinda wa Bayern Munich Renato Sanchez.
Chelsea baada ya kumsaini Bakayoko inasemekana wanakaribia kufanya usajili mkubwa mwingine kwa kumleta Mgabon Pierre Aubemayang ambaye inahitajika £65m kumng’oa Borussia Dortmund.

No comments