Header Ads

Tetesi za usajili barani Ulaya hii leo


Benjamin Mendy amesafiri kuelekea jijini Los Angeles ambako anakwenda kufanya vipimo vya afya tayari kujiunga na klabu ya Manchester City uhamisho ambao utaigharimu klabu ya Manchester City kiasi cha £52m.
Klabu ya Manchester United imeamua kuachana na mpango wa kumnunua kiungo wa PSG Marco Verrati baada ya klabu ya PSG kudai mabadilishano kati ya Verrati na Martial deal ambalo United wamelikataa.
Katika kuonesha wamepania kumchukua Phillipe Coutinho, klabu ya Barcelona imeongeza dau lao hadi kufikia £82m ili kupata saini ya kiungo huyo wa Kibrazil.
Baada ya kumtambisha mlinzi Kyle Walker aliyetoka klabu ya Tottenham sasa leo Manchester City leo wamemtambulisha beki wa Real Madrid Danilo ambaye amesaini kwa dau la £26m.
Klabu ya As Roma imeshafanya makubaliano binafsi na winga wa Leicester City na sasa kinachosubiriwa ni vilabu hivyo viwili kufanya makubaliano tayari kwa Mualgeria huyo kwenda kukipiga nchini Italia.
Manchester United wanaaamini wanaweza kumnunua Nemanja Matic kutoka Chelsea baada ya Bakayoko kutua Chelsea,gharama za kumtoa Matic Chelsea inaweza kuwa £50m au zaidi.

No comments