Header Ads

Sababu kwanini Juve wamemuuza Bonucci, kisa cha kuzikataa Chelsea & Man City


Uhamisho wa Leonardo Bonucci kutoka Juventus kwenda AC Milan kwa ada ya uhamisho wa 40 million euros ni moja ya biashara iliyoistua ulimwengu wa soka. 
Tunaongalia kutoka nje tunashindwa kuelewa ni namna gani mmoja wa walinzi bora kabisa katika kizazi hiki, ambaye aliisaidia Juve kuunda ukuta wa Turin, ameruhusiwa kuondoka kwa bei ambayo kwa soko la sasa inaonekana ndogo. 
Bonucci hajaondoka tu Juventus, ila ameondoka kwenda kujiunga na klabu pinzani ya Italia inayoshiriki katika Serie A. 
Kwa beki wa kati wa aina yake, kuondoka Juventus – timu ambayo imeshinda Serie A mara 6 mfululizo, na kwenda kujiunga na timu inayocheza katika Europa League katika msimu ujao – ni jambo la kushangaza kidogo. 
Nchini Italy,  kuna mashaka mengi juu ya ada iliyolipwa. Pamoja na kuwa na miaka 30, mchezaji huyo wa Azzurri bado ni mmoja yupo kwenye Top 5 ya mabeki bora wa kati duniani.  
Chelsea walilipa 50m euros kumsajili David Luiz msimu uliopita na Manchester City walitumia jumla ya 128m euros kuwasaini mabeki wao John Stones, Nicolas Otamendi na Eliaquim Mangala – wachezaji hawa wote hakuna anayemsogelea Bonucci kwa ubora. 
Mahusiano mabaya 
Moja ya sababu kuu iliyosababisha Bonucci kuondoka Juventus ni mahusiano mabaya na kocha Massimiliano Allegri. Wakati wa mchezo wa ushindi wa magoli 4-1 dhidi ya Palermo msimu uliopita, Bonucci na Allegri, kocha huyo alimtolea kauli mbaya mchezaji wake kwa kumwambia: ‘Shut up you d******d. Go f**k yourself!’
Wakati wachezaji wenzake wakishangilia ushindi na mashabiki wa nyumbani, Bonucci aliondoka haraka kuelekea chumba cha kubadilishia nguo baada ya kujibishana, na matokeo yake akapigwa chini katika kikosi cha Champions League dhidi ya Porto. 
Baada ya hapo, wote wawili walikubaliana kuweka tofauti zao pembeni kwa ajili ya manufaa ya timu angalau mpaka mwishoni mwa msimu, huku ikionekana wazi Bonucci angeondoka. 
Kwanini Milan?
Hata hivyo, swali kubwa kwanini hakuhamia katika ligi kuu ya Uingereza? La Gazzetta dello Sport wameripoti kwamba Chelsea na  Manchester City walikuwa tayari kulipa zaidi ya €50m kupata saini ya Bonucci. 
Kwa Bibi Kizee cha Turin, ingekuwa bora kwao kumuuza mchezaji wao kwa klabu ya nje na kutokuja kukutana kwenye ligi. 
Kwasababu za kifamilia, hasa ukizingatia hali ya afya ya mwanae wa kiume ambaye ni mgonjwa, Bonucci hakutaka kuondoka nchini kwao na hivyo akachagua kujiunga na timu nyingine ya Serie A, huku Milan ikiwa ndio timu pekee iliyoonyesha nia ya kumsaini. 
Nini kinafuata kwa Juve? 
Hakuna mwenye shaka kwamba pengo la Bonucci litakuwa gumu kuzibika lakini hata msimu uliopita, Allegri alikuwa akitafuta namna kufanya maboresho ya safu ya ulinzi iliyokuwa na umri mkubwa ikiwahusisha Dani Alves (34), Bonucci (30), Giorgio Chiellini (32) na Andrea Barzagli (36), wote kwa pamoja wakiwa na umri wa miaka 132. 
Kuondoka kwa Bonucci na Alves kunamruhusu  Allegri kumtumia kinda wa miaka 22 Daniele Rugani kuziba pengo hilo. 
Juventus pia ni klabu tajiri wana uwezo wa kusajili kama walivyofanya msimu uliopita kwa  Gonzalo Higuain – uhamisho huu walichukua fungu kutoka kwenye mauzo ya Pogba.
Safari hii, mauzo Bonucci yanewaruhusu kumsajili Douglas Costa kutoka Bayern Munich kwa ada ya 42m euros.

No comments