Header Ads

Pedro ajipa moyo kuhusu Diego Costa, asema akiondoka ni janga


Ni mvurugano juu ya mvurugano kwani hali kati ya mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa na kocha wake Antonio Conte sio nzuri hata kidogo na wawili hao hawako sawa kwa sasa.
Taarifa za mwanzo zilisema Antonio Conte alimuambia Diego Costa kupitia ujumbe mfupi wa simu kwamba hamtaki katika klabu hiyo na wala hayupo kwenye mipango yake.
Baada ya taarifa hizo kuzagaa ilimbidi Costa kuanza kujua nini hatma yake ndani ya Chelsea huku ikiripotiwa kwamba mshambuliaji huyo ameshaanza kutafuta klabu mpya.
Sasa mchezaji wa klabu hiyo Pedro Rodriguez ana yake kichwani kuhusu Costa, Pedro anajipa moyo kwamba Costa atabaki nao katika msimu ujao wa ligi na hataenda popote.
“Ni muhimu sana kwetu Diego kwani amefunga karibia katika kila mechi zetu na ni mshambuliaji wetu ambaye mabeki wanamuhofia kucheza dhidi yake” alianza Pedro.
“Diego anakupa nguvu ya ziada maana ana kipaji,ana nguvu na anafunga,kama akiondoka litakuwa tatizo kubwa sana kwetu lakini sisi kama marafiki zake tunatamani aendelee kubaki” alisema Pedro.
Kwa sasa inaonekana imekuwa ngumu kwa Chelsea kununua mshambuliaji mkubwa kuziba nafasinya Diego hadi sasa, jambo ambalo linaweza kuwafanya wamshawishi Costa kubaki.


No comments