Header Ads

Nawachukia wanaokwepa kulipa kodi -Rais Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amesema kuwa anawachukiwa sana wanaokwepa kulipa kodi huku akisema kuwa serikali haina shamba inategemea kodi za wananchi.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo wakati anahutubia wananchi katika uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya Kibondo-Nyakanazi yenye KM 50.
“Serikali haina shamba, inategemea kodi za wananchi na ndio maana nawachukia sana wanaokwepa kulipa kodi, nawanaokwepa kulipa kodi ndugu zangu niwaeleze sio wananchi wa kawaida, ni wale matajiri wakubwa wakubwa ndio wanaokwepa kulipa kodi kwa mfano nyinyi le mkipanda kwenye basi lile basi mlilipia kodi wakati wa kununuliwa hata likienda kunywesha mafuta, nauli ile uliyoilipa unakuwa umeshalipa kodi kwaajili ya mafuta,” amesema Rais Magufuli.
“Yale ni jukumu tu la wale wenye vituo vya mafuta lipia ile kodi mliyoikusanya waende wailipe serikalini lakini wapo wenye vituo vya mafuta ambao umelipa kodi wanabaki nazo kodi kana kwamba ni kodi zao, hao ndio ninataka kulala nao mbele. Nimetoa siku 14 na sasa sijui zimebaki siku 12 sijui 13.”

No comments