Header Ads

Maskini Michu, alazimishwa kustaafu soka awaachia mashabiki ujumbe wa kusikitisha


Unamkumbuka Michu?mwaka 2012 aliponunuliwa tu Swansea kila mtu alianza kumzungumzia haswa baada ya kufunga mara 2 wakati Swansea wakiilaza Arsenal kwa bao 2 kwa 0.
Timu zote kubwa Uingereza zinamkumbuka,ameshawafunga Arsenal,Manchester zote mbili akawafunga Chelsea na msimu wa mwaka 2012/2013 akaumaliza na mabao 22.
Pamoja na kumaliza nafasi ya 9 lakini Michu aliisaidia Swansea kubeba kombe la Capital One ambalo ndio kombe lao kubwa kuwahi kubeba katika historia yao.
Majanga yakaanza kuja baada ya Michu kurudi Hispania kukipiga katika klabu ya Real Oviedo inayoshiriki ligi daraja la pili nchini Hispania hapo kila kitu kikabadilika.
Majeraha yakaanza kumuandama Michu mwenye miaka 31 na akacheza michezo 12 tu tangu ajiunge na klabu hiyo ya Real Oviedo inayoshiriki Segunda Division.
Ripoti ya madaktari inasema Michu hawezi kuendelea kucheza “taarifa za kitabibu zinasema matatizo yangu ya enka yatanilazimu kusema kwaheri katika ulimwengu wa soka”
“Naumia sana kuaga lakini naamini mutabaki mukiwa wamoja,nasema ahsante kutoka ndani ya moyo wangu hakika mumekuwa na mimi katika kipindi chote,ahsanteni”
“Najisikia faraja kutimiza ndoto zangu za kucheza soka katika ngazi ya juu lakini ninyi mumekuwa mhimili mkubwa sana kwangu na sina cha kuwalipa,asanteni na kwaherini” amesema Michu kupitia taarifa aliyoitoa Twitter.

No comments