Klabu ya Manchester City imekubali kutoa kitita cha pauni millioni 50 kwa ajili ya kupata huduma ya beki wa kulia wa Tottenham Kyle Walker kwa ajili ya kuitumikia klabu hiyo ya jijini Manchester na anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya siku ya ijumaa.
Image result for kyle walker
Kocha Pep Gurdiola yupo kwenye harakati ya kukijenga upya kikosi chake cha City baada ya kuwatimua baadhi ya wachezaji wakiwemo Pablo Zabaleta,Gael clichy na Bakar Sagna na usajili wa Walker utakuwa ni watatu baada ya kufanikiwa kumsajili Bernardo Silva na goli kipa Ederson Moraes.
Image result for kyle walker
Usajili wa Walker utakuwa usajili ghali zaidi duniani kwa upande wa mabeki huku mchezaji huyo akiwa na umri wa miaka 27,Akiwa Hotspurs Walker alifanikiwa kuchaguliwa kati ya wachezaji waliotajwa katika kikosi bora cha msimu uliopita,Walker alijiunga na Tottenham mwaka 2009 kutoka sheffield United na mpaka sasa ameichezea Tottenham michezo 200.
Walker helped Tottenham achieve their highest finish in the top flight since the 1960s