Ajali ya ndege yauwa watu 16
Watu 16 wamefariki papo hapo kwenye ajali ya ndege ya jeshi huko Mississipi nchini Marekani.

Mabaki ya Ndege yakiteketea kwa moto
Ajali hiyo ilitokea katika Kaunti ya LeFlore karibia kilomita 160 kusini mwa mji mkuu wa jimbo hilo, Jackson.
Kwa mujibu wa mtandao wa Shirika la utangazaji la Reuters Watu wote 16 waliokuwa ndani ya ndege hiyo waliangamia huku chanzo cha ajali kikiwa bado hakijafahamika.
Hata hivyo jarida la kiserikali la jimbo la Mississipi limeandika kuwa ndege hiyo ilianguka katika shamba moja na mabaki yake kutapakaa maeneo tofauti tofauti.
Ndege hiyo yenye namba KC-130 ni moja ya ndege za kijeshi zenye gharama kubwa zinazotumiwa na Jeshi la majini la Marekani kwenye nyakati tofauti.

Mfano wa ndege iliyopata ajali KC-13J Marines
Kupitia ukurasa rasmi wa twitter wa Jeshi la Majini wamethibitisha taarifa hizo huku wakieleza kuwa taarifa zaidi zitatolewa kesho kuhusu ajali hiyo.
Post a Comment