Header Ads

£75m, miaka 24, mabao 25 Lukaku ni usajili usio na shaka kwa United


Mwaka 2014 alikuwa ni kocha Jose Mourinho ndiye alihitimisha uhusiano wa Chelsea na Lukaku baada ya kocha huyo kumuondoa Lukaku toka The Blues akisema bado hakuwa hatari lakini kuanzia hapo Lukaku kiwango chake kikawa kinakua.
Sasa miaka mitatu imepita toka Mourinho amuuze Lukaku na sasa anamnunua kwa kiwango kikubwa sana cha pesa zaidi ya £75m na anamnunua katika kipindi ambacho kwa hakika anahitaji mtu aina ya Lukaku kuja kuokoa jahazi la United.
Msimu uliopita alikuwepo Zlatan Ibrahimovich ambaye kiuchezaji ana tofauti na Lukaku kwani Zlatan alikuwa akisimama tu karibia na goli ili kumalizia mipira inayokuja lakini Zlatan hakukidhi kwa 100% kilichokuwa kikitarajiwa na United toka kwake.
Pamoja na kufunga mabao mengi lakini Zlatan pia alipoteza nafasi nyingi, United walihitaji mshambuliaji na sio tu mshambuliaji walihitaji mshambuliaji mwenye vitu vingi katika miguu yake kama ilivyokuwa kwa Wayne Rooney alipokuwa kijana mdogo.
Hakuna ubishi kuhusu uwezo wa Lukaku, ni mshambuliaji ambaye ana kila kitu ambacho mshambuliaji anapaswa kuwa nacho,anakimbia,ana skills na ni muuaji wa nyavu, ni aina ya washambuliaji wanaoweza kukupa matokeo katika nyakati ngumu.
Msimu uliopita alifunga mabao 25 na uzuri mabao hayo alifunga 7 kwa mguu wa kulia na 12 kwa kushoto na kumfanya awe kinara wa kufunga kwa guu la kushoto kitu kinachoonesha uwiano mzuri wa miguu yake na huku mabao 6 akifunga kwa kichwa, ni dhahiri Lukaku anatumia vyema kila kiungo kucheka na nyavu.
Ligi ya Epl ni ngumu na kwa mtu aliye chini ya umri wa miaka 25 kama Lukaku ni jambo kubwa sana kufunga mabao zaidi ya 10 katika misimu mitano mfululizo na hii inawapa United matumaini kwamba hawawezi kosa mabao “double figure 10+” toka kwake.
Kucheza mbele ya Juan Mata, Mkhitaryan na Paul Pogba hakika inaweza kuwa kilio kwa timu pinzani, aina za movements za Lukaku anapokuwa uwanjani huwa zinawasumbua sana mabeki na uwepo wa viungo waliopo Manchester United inaweza kuzidisha uhatari wa Lukaku.
Kutokana na umri wa Romelu Lukaku wa miaka 24 na uwezo wake wa kufunga nadhani dau lake ni sahihi kabisa na halina mashaka hata kidogo kama linavyozungumziwa, kwa mshambuliaji ambaye kila msimu anafunga mabao zaidi ya 10 na bado ni kijana mdogo £75m ni sahihi kabisa haswa katika soka hili la pesa.

No comments