Z, ANTON nina fremu 70 za biashara
Msanii wa muziki, Z Anto amefunguka kwa kudai kuwa yeye ni mfanyabisha mkubwa ambaye anamiliki zaidi ya fremu 70 za biashara.
Z AntoMuimbaji huyo ameiambia hamisi hemedi.com kuwa kwa muda mrefu amekuwa akijihusisha na biashara tofauti tofauti akiwa nje ya muziki.
“Mara nyingi wasanii wana maneno mengi pasipo vitendo, ningekuwa karibu katika mazingira yangu ya biashara ningekwambia angalia aina ya biashara ambayo nafanya. Mimi ni mmliki wa fremu za biashara kama 70 na kitu hivi,” alisema Z Anto.
Aiongeza, “Lakini pamoja na hilo pia na biashara nyingine ambazo nafanya na kila siku naendelea kutafuta biashara mpya za kufanya,”
Katika hatua nyingine muimbaji huyo amedai kwa sasa anajipanga kuitambulisha kampuni yake mpya itayokuwa inasimamiwa muziki wake.
Post a Comment