USAJILI: Yanga SC yamtema Haruna Niyonzima
Mchezaji wa klabu ya Yanga SC, Haruna Niyonzima
Klabu ya soka ya Yanga SC imetoa taarifa ya kuachana na aliyekuwa mchezaji wake wa kimataifa raia wa Rwanda, Haruna Niyonzima baada ya kushindwa kuafikiana.
Na hii ni taarifa kutoka ndani ya uongozi wa klabu hiyo.
Yanga SC kupitia kwa Katibu Mkuu Boniface Mkwasa inapenda kuwajulisha wanachama, wapenzi na washabiki wa Yanga juu Mchezaji raia wa Rwanda Haruna Niyonzima ambaye amekua Mchezaji wetu kwa misimu 6 mfululizo katika kiwango cha juu.
Hata hivyo Haruna Niyonzima bado ana mkataba mpaka mwezi Julai na Yanga Sc, lakini hatutaweza kuendelea kuwa nae kwa msimu ujao kwani hatukuweza kufikia mwafaka katika mazungumzo yetu na yeye licha ya timu yetu kuwa na nia za kuendelea nae kwa misimu miwili ijayo.
Klabu inamtakia kila la kheri katika maisha yake na soka kwa ujumla.
Imetolewa na Idara ya Habari na Maelezo
Young Africans Sports club.
21-06-2017.
Post a Comment