Ujumbe wa Vanessa Mdee kwa Jux, atupa dongo gizani
Ni jambo zuri ukiona mtu wako wa karibu amefanikisha moja ya ndoto zake
katika maisha yake. Ni muhimu kumpatia ujumbe ambao utakaomtia moyo
katika kufanikisha mambo yake mengine aliyoyapangilia.
Vanessa Mdee ameamua kutumia vizuri fursa hiyo katika kumpongeza
mpenzi wake Jux ambaye amehitimu masomo yake huko nchini China. Lakini
katika ujumbe huo pia Vee amewapiga dongo watu waliokuwa wakimkejeli
mwenza wake huyo kutokana na muimbaji huyo kutoonyesha picha yoyote
akiwa na wanafunzi wenzake.Kupitia mtandao wa Instagram, Vanessa ameandika:
Congratulations @juma_jux U finally done ✅ and you done did it well. Hapo watu walikuwa wakiombaga picha za wewe darasani nadhani hii picha jibu la kutosha. Umeweza kufanya yote, MZIKI, BIASHARA NA SHULE… now that’s exceptional. Muda wa vibunda babaaa. Keep inspiring the YUTEEEEE 🙌🏾👌🏾🎊
Post a Comment