Sumaye aiangukia Serikali, aomba kuivumilia Chadema
Waziri
Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye amefunguka na kuitaka serikali ya awamu
ya tano iwavumilie na itambue kuwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) pamoja na viongozi wake ni chama halali kinafanya kazi kama
CCM inavyofanya kazi zake.
Sumaye
aliyasema hayo jana baada ya jeshi la polisi kuzuia msafara wao ambao
ulikuwa na lengo la kutembelea na kujionea utendaji kazi wa Manispaa ya
Ubungo inayoongozwa na CHADEMA.
"Hili
si jambo la ajabu kwa sababu hata viongozi wa CCM kwa mfano hata Pole
Pole anazunguka halmshauri zote nchini, ila wanapozunguka wao hakuna
tatizo ila inapokuja viongozi wa CHADEMA kidogo tayari wanaanza
mapambano, tunadhani huu ni uonevu tu unaendelea wa kujaribu kuwafanya
watu wengine wajisikie kwamba hawana uhuru na nchi yao hili nafikiri si
jambo jema.
"Serikali
tunaomba ituvumilie ijue kwamba CHADEMA pamoja na viongozi wake ni
chama halali kinafanya kazi kama CCM wanavyofanya kazi kwa hiyo mambo ya
kuandamwa CHADEMA kila mahali inatusikitisha sana" alisema Sumaye
Mbali
na hilo Sumaye anasema vitendo hivyo vinavyofanywa kwa viongozi wa
CHADEMA ni kutaka kukatisha tamaa jitihada zozote zinazofanywa na
viongozi wa chama hicho hivyo anadai ni kitu ambacho hakiwezi
kuvumilika.
"Kwa
jambo hili mimi nataka tu kuimbia serikali kuwa hawatafanikiwa kwani
wataleta vurugu pasipo kuwa na sababu zozote zile, wawaache watu wafanye
kazi zao hapa hakuna siasa zozote tunazofanya.
"Tunakagua
miradi kwani halimashauri hizi ni zetu kama ambavyo wao wanatembea
kwenye halimashauri zote nchini kuona namna Ilani yao inavyotekelezwa na
sisi tunataka kujua viongozi wetu wa CHADEMA wanatekeleza vipi yale
ambayo CHADEMA imewaagiza kufanya katika Ilani yake. Na miradi hii ni
kwa wananchi wote" alisisitiza Sumaye
Post a Comment