SORRY MADAM -Sehemu ya 66 & 67 (Destination of my enemies)
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWAILIPOISHIA
ILIPOISHIA
Ukelele
wa kulia kwa uchungu ulio tokea juu kabisa ya gorofa ukawafanya wote
watatu kustuka hususani Shamsa ndio alishtuka zaidi, akajitoa mikononi
mwa madam Mery na kuanza kukimbilia kuelekea gorofani, huku Madam Mery
na Sa Yoo wakimfwata kwa nyuma. Wote watatu wakamkuta Black Shadow akiwa
amepiga magoti chini, akilia kama mtoto huku sura yake akiwa
ameiinamisha kwenye mwili wa Sabogo ulio lala chini kwa kunyooka
ukishiria kwamba Sabogo amepoteza maisha.
“Babyyyy……..”
Shamsa
aliita huku akikimbilia sehemu alipo Black Shadow, na kuwaacha Sa Yoo
na Madam Mery wakiwa wamesimama wasijue ni nini cha kufanya.
ENDELEA
Shamsa
akazidi kumsogelea Black Shadow, taratibu akamgusa begani jambo lililo
mfanya Black Shadow kujiifikiria kwa muda kabla hajainyanyua sura yake
kwa maana anamtambua vizuri Shamsa kwamba ni mwanae wa kumlea japo
Shamsa hatambui ukweli wa aina yoyote.
‘Liwalo na liwe’
Black
Shadow alizungumza huku taratibu akinyanyua kichwa chake kutoka katika
mwili wa Sabogo aliye iaga dunia kwa kupigwa risasi na Lee Si. Taratibu
Black Shadow akaigeuza sura yake na kumtazama Shamsa aliye stuka na
kuyatoa macho yake, mstuko huo haukuwa kwa Shamsa peke yake, bali Madam
Mery pamoja na Sa Yoo nao wakabaki wakimkodolea macho Eddy kwani wote
walili wanamtambua vizuri hususani madam Mery aliye kuwa mwalimu wa Eddy
tangu akiwa kijana mdogo.
“EDDY………”
Shamsa
aliita huku akiwa bado hayaamini macho yake, mwili mzima Shamsa akahisi
unamuishia nguvu. Taratibu Shamsa akajikuta akianguka kwenda chini,
kabla hajafika chini Eddy akamdaka, Shamsa akazimia.
“Shamsa, Shamsa, Shamsaa”
Eddy
alimuita Shamsa ila hakuitika kwa haraka Eddy akamnyanyua Shamsa na
kumuweka begani mwake na kuanza kutoka kushuka kwenye jengo hilo huku
Madam Mery na Sa Yoo wakifwata kwa nyuma wote wakionekana
kuchanganyikikwa. Wakafika chini Eddy akataka kupanda pikipiki yake, ila
Sa Yoo akamuomba watumie gari ambalo walikuja nalo.
“Lete funguo”
Eddy
alizungumza mara baada ya kumuingiza Shamsa ndani ya gari, Sa Yoo
akamkabidhi Eddy funguo na wote wakaingia kwenye gari, wakaondoka eneo
hilo. Hapalukwa na mtu aliye weza kuzungumza kitu cha aina yoyote, kila
mmoja alimfikiria Shamsa aliye laza kichwa mapajani mwa Madam Mery huku
Sa Yoo akiwa siti ya mbele mara kwa mara aligeuka nyuma kuwez
akumuangalia Shamsa.
“Unaelekea wapi?”
Sa
Yoo aliuliza baada ya kuona wanaelekea nje ya mji. Eddy hakujibu kitu
chochote zaidi ya kuongeza mwendo kasi wa gari hadi wakafika kwenye
msitu mmoja mkubwa. Eddy akakunja kushoto kwenye barabara ndogo iliyo
jaa nyasi nyingi. Akaongeza mwendo kasi hadi wakafanikiwa kufika kwenye
pango kubwa, ambapo Eddy kwa haraka akshuka kwenye gari na kumtoa
Shamsa, akambeba begani, Madam Mery na Sa Yoo wakamfwata kwa nyuma
pasipo kuuliza ni wapi wanapo ingizwa.
Madam
Mery na Sa Yoo wakaonekana kushangaa mazingira ya ndani ya pango hilo
lililo jengwa kwa ndani vizuri na kuna taa nyingi ambazo zinapendezesha
mandhari ya ndnai ya pango hilo.
Eddy
akamlaza Shamsa kwenye moja ya sofa, lililopo sebleni. Akamfungua
kifungo cha suruali yake kisha akamvua tisheti aliyo vaa akabakiwa na
sidiria.
“Mpeni muda wa kupumzika amepoteza fahamu huyo”
Eddy
alizungumza huku jasho likimwagika usoni mwake, akashusha punzi na
kuanza kuwatazama Madam Mery pamoja na Sa Yoo binti aliye msaidia
kipindi anatafutwa na askari wa hapa nchini Japan.
“Kweli wewe ndio Black Shadow?”
Sa Yoo aliuliza huku macho yake akiwa amemtumbulia Eddy.
“Ndio mimi”
Eddy
akamtazama Madam Mery ambaye anaonekana anajambo ambalo anahitaji
kuzungumza ila anashindwa kulizungumza kwa wakati huo kutokana na uwepo
wa Sa Yoo. Eddy baada ya kuligundua hilo akaanza kutembea kuelekea nje
na Madam Mery akamfwata kwa nyuma.
“Umefikaje huku?”
Eddy
alimuuliza Madam Mery kwa sauti nzito iliyo jaa hasira ndani yake, kwa
maana kumbukumbu ya chanzo cha mtu aliye haribu maisha yake, ikamjia
Eddy kichwani na Madam Mery ndio muhusika mkuu wa maisha ya Eddy
kuharibika wakishirikiana na Mzee Godwin.
Taratibu
Madam Mery akapiga magoti chini, huku machozi yakimwagika, kwani
anamuelewa Eddy vizuri na anatambua hali aliyo kuwa nayo kwa sasa ni
hali ya hasira na endapo atazungumza jambo baya basi maisha yake yapo
hatarini kuondoka.
“Eddy,
ninahaki ya kufa mikononi mwako, nipo tayari hata sasa hivi maisha
yangu yatoke, ila nina kitu kimoja ninahitaji kuzungumza na wewe kabla
hujaniua”
Madam
mery alizungumza kwa sauti ya unyonge, machozi yakiendelea kumwagika
usoni mwake. Kitendo cha sauti ya Madam Mery kupenya masikioni mwa Eddy
kikazidisha hasira yake na kujikuta akikunja ngumi, mkono wa kulia huku
mmkono wa kushoto ukimtetemeka sana.
“Sinto
hitaji kusikia kitu chochote kutoka kwako, niliyaacha maisha yako kwa
mara ya kwanza kwa kuheshimu msiba wa mke wangu, mwanangu na mama yangu.
Ila kwa sasa nitakuua kisha atafwata Godwin”
Eddy
alizungumza huku akimgeukia Madam Mery aliyepiga magoti pembeni yake.
Akatamani alichomoe koo la Madam Mery kwa mkono wake wa kushoto unao
tetemeka kwa hasira, ila akajikuta mkono huo ukiwa ni mzito sana kufanya
jambo hilo. Madam Mery akatulia kimya, huku macho yake ameyafumba kwani
anatambua ni nini anacho stahili kufanyiwa. Zikapita sekunde kadhaa za
ukimya, Madam Mery akayafumbua macho yake na kumuona Eddy akiwa
anaondoka kuingia ndani ya pango hilo na hajamfanya kitu chochote.
“Eddy tunatakliwa kumuua Godwin”
Eddy
akasimama, kisha akageuka taratibu na kumtazama Madam Mery aliye piga
magoti. Macho ya Eddy yaliyo jaa uwekundu wa hasira huku kwa mbali
yakilengwa lengwa na machozi ya hasira, yakaanza kumpandisha na
kumshusha madam Mery. Kisha sauti mbili moyoni mwake zikawa zinabishana
kwenye kufanya maamuzi. Sauti yake ya kwanza inamtuma kumuua madam Mery
muda huo huo, huku sauti yake ya piliikimuomba asifanye mauaji ya mwana
mama huyo na amsikilize kwa kile ambacho Madam Mery anahitaji kumuambia.
“Tanzania pamoja na raisi Praygod wapo matatani, muda wowote na saa yoyote wanaweza kupoteza maisha……”
“Kutokana Godwin amekuwa……….Raisi wa nchini Tanzania”
“NINI…..?”
Eddy
alistuka sana kusikia habari hiyo ambayo ni mbaya sana ndani ya masikio
yake. Akamfwata Madam Mery kwa kasi hadi sehemu alipo piga magoti,
jambo lililo mfanya madam Mery ajikute amekaa chini kutokana na
kumuogopa Eddy.
“Umesemaje………..?”
“Ni…nini….memee..eeesema baa…ba yak…o Go…d……win amekuwa raisi wa Tanzania”
Madam
Mery alizungumza huku mwili mzima ukimtetemeka, japo kuna baridi Eddy
akajikuta jasho likimwagika kwa hasira. Kila alicho kifikiria juu ya
Mzee Godwin kilimchanganya akilini mwake.
“Na Phid….aya bado yupo hai”
Maneno
ya Madam Mery yakazidi kumumshangaza Eddy akilini mwake na kuanza
kumkumbuka Nesi Phidaya ambaye alimfananisha na mke wake ila kitu
kilicho mchanganya ni kwamba tayari alisha mzika mkewe Phidaya.
***
Matajario mazuri ya watanzania juu ya uongozi wa Raisi Godwin, yakaanza
kupotea kadri siku zilivyo zidi kwenda. WWengi walitarajia ugumu wa
maisha utapungua ila ndio kwanza ukazidi kuongezeka mara kumi ya awali
walivyo kuwa.
Nchi
haikuwa ya watanzania wote bali, ikageuka kuwa nchi ya watanzania
wachache, wenye nguvu ya kipesa na wenye maamuzi ya kufanya chochote kwa
wakati wowote na kwamtu yoyote. Uonevu ukazidi kuongezeka kwa wananchi
wa hali za chini, watu wote walio msaidia mzee Godwin kuingia
madarakani, walikabidhiwa madaraka makubwa ambayo, hata watu wengine
walio kua katika serikali ya raisi Praygod na kumuunga mkono, waliweza
kupigwa chini, huku baadhi yao wakibambikiwa kesi na kusekwa magerezani,
huku wengine wakifilisiwa na kubaki kuwa masikini kabisaa.
“Mzee tunatakiwa kidogo tuwajali wananchi, hata miaka mingine mitano ukigombania uraisi wakupatie kura zao”
Mshauri
wa raisi wa Mzee Godwin, alizungumza huku akimtazama raisi Godwin usoni
mwake. Mzee Godwin akatabasamu kidogo kisha akaachia kicheko cha dharau
na kumtazama mshauri wake bwala Mgwira
“Ni nani aliye kudanganya kwamba kutakuwa na kupiga kura tena nchini Tanzania?”
“Una maana gani muheshimiwa?”
“Maana
yangu ni kwamba hakuna mtu ambaye atanitoa madarakani kwa kupiga kura.
Hii nchi kwa sasa ni yangu na nitaiongoza hadi pale nitakapo fariki na
endapo itatokea nitakufa basi atakaye tawala atakuwa ni Manka mwanangu
kipenzi”
Bwana Mgwira akabaki amemtumbulia macho mzee Godwin, anaye zungumza kwa kujiamini sana.
“Nahitaji nchi hii nibadilishe mfumo wa utawala, uwe utawala wa kifalme na si utawala wa kiraisi”
“Muheshimiwa……………..!!!”
“Ndio, na tena wasiliana na viongozi wote kesho ninahitaji kufanya nao mkutano sawa”
“Sawa muheshimiwa”
Mzee
Mgwira hakuwa na kitu cha kuzungumza zaidi ya kukubaliana na raisi
Praygod ambaye siku zote akizungumza haitaji mtu yoyote aweze kukipinga.
Manka akaingia kwenye sebule ya baba yake na kumkuta akiwa amekaa na
Mzee Mgwira, ambaye baada ya kumuona Manka akanyanyuka na kuondoka,
kuwapisha baba na mwana kuzungumza.
“Baba mbona unaonekana leo una furaha sana?”
“Ninafuraha mwanangu kwa maana nimefikiria kitu ambacho nina imani kitakuweka wewe kwenye mazingira mazuri sana”
“Kitu gani hicho baba, wakati unamiliki kila kitu kwa sasa?”
“Ninakwenda kubadilisha mfumo wa serikali kutoka katika mfumo wa serikali ya uraisi na kuingia katika serikali ya ufalme”
Mzee Godwin alizungumza huku akifurahia sana.
“Ufalme, ufalme wa aina gani?”
“Nahitaji
kuwa mfalme, nitakuwa nikiongoza katika maisha yangu yote na hata mimi
nikifa basi wewe mwanangu utatawala katika kiti cha ufalme na utakuwa ni
malkia”
Manka
naye aklajikuta akitabasamu na kufurahi sana, juu ya wazo ambalo baba
yake amelifikiria. Kwa nguvu walio kuwa nayo walijiamini kwamba kila
kitu ndani ya Tanzania ni chakwao.
“Wezako wanaendeleaje?”
“Wapo salama tu, kila mtu anaendelea na majukumu yake kwenye wizara ambayo umewapatia”
“Basi wasiliana nao na kesho uwaambie kwamba nina kikao ambacho kitakuwa kinakwenda kuihalalisha serikali ninayo ifikiria”
“Sawa baba”
Manka
akanyanyuka kwenye sofa alilo kalia akamsogelea baba yake na kumbusu
shavuni na kuondoka zake sebleni na kumuacha Mzee Godwin akifikiria
mambo yake.
Siku iliyo fwata, mkutano wa viongozi wote ndani ya serikali ya Mzee
Godwin wakakutana kwenye kikoa ambacho kila mmoja alishangazwa na ukubwa
wa kikao hicho kwa maana tangu uongozi wa raisi Godwin uanze hajawahi
kuitisha kikao kikubwa kama hicho.
“Habari za asubu”
Raisi
Godwin alizungumza kupitia kipaza sauti kilichopo kwenye meza yake,
kila kiongozi aliye kuwepo kwenye eneo hilo aliitikia. Raisi Godwin
akawatizama viongozi walio chini yake kisha akakohoa kidogo na kuanza
kuzungumza kitu ambacho alikusudia kukizungumza.
“Ninahitaji kubadilisha mfumo wa serikali”
“Serikali
ambayo ninahitaji iwe kwa sasa, itakuwa ni serikali ya ufalme, na hili
swala sinto hitaji mtu wa iana yoyote kuweza kulipinga hili”
Minong’ono
ya chini chini ikaanza kutawala ndani ya chumba cha mkutano, kila mmoja
aliweza kuzungumza chake juu ya kitu kilicho zungumza na Raisi Godwin.
“Kuna baadhi ya sekta nitazifuta rasmi kuanzia leo na sekta ya kwanza itakuwa ni Tume ya taifa ya uchaguzi”
“Eheee bwana Luka unahitaji kuzungumza nini?”
“Muheshimiwa
raisi wazo lako ulilo litoa si baya, ila itakuwaje kwa hao wananchi
ambao tuna waongoza, watakubaliana kweli na hili?”
“Jeshi tunalo, nguvu ya pesa tunayo ni nani anayewezakupinga kauli yangu?”
Raisi Godwin alizungumza na kuwafanya viongozi wote kuwa kimya wasizungumze neno la aina yoyote.
“Ninaagiza waziri wa mawasiliano, vijulishe vyombo vya habari namuwatangazie juu ya hili nililo zungumza sawa”
“Sawa mkuu”
“Na
kitu cha mwisho ambacho labda nitawahurumia wananchi wangu, waweze
ku[iga kura za ndio na hapana kupitisha serikali ninayo itaka na watakao
kataa. NITAJUA NI NINI CHAKUFANYA”
Post a Comment