Header Ads

Shamsa Ford Aiweka Rehani Ndoa Yake!

STAA ‘upper class’ katika kiwanda cha filamu Bongo, Shamsa Ford ‘Chausiku’ amesema miongoni mwa mambo ambayo aliyabeba moyoni na kuyaombea dua maalum katika kipindi chote cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni pamoja na uhai wa ndoa yake, hivyo anamuachia Mungu atende sawasawa na maombi yake.

Katika mazungumzo na Star Mix msanii huyo mwenye uwezo wa ‘makinikia’ linapokuja suala la kuigiza, aliweka wazi kuwa kama mwanadamu haishiwi na mapungufu ambayo ameyatubu kwa Mungu.

“Kama binadamu siishiwi na makosa, lakini katika mfungo huu wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, yapo mengi ambayo niliyafanyia toba maalum, lakini kubwa sana ni uhai wa ndoa yangu, maana siko tayari kwa kweli kuvurugikiwa na kuvunjika kwa ndoa hii ambayo inamaanisha furaha ya maisha yangu, kwa hiyo naiweka ndoa yangu kwa Mungu na yote namuachia yeye,” alisema Shamsa.

No comments