Header Ads

Real Madrid yatwaa ubingwa wa UEFA 2017

 
Klabu ya Real Madrid ya nchini Uhispania imeichakaza Juventus ya Italia 4-1 na kushinda Kombe la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya huku ikiweka rekodi ya kuwa  klabu ya kwanza kuchukua ubingwa mara mbili mfululizo.
Mreno Cristiano Ronaldo alifunga mabao mawili, la kwanza kwake na klabu dakika ya 20 na lake la pili dakika ya 64.
Casemiro aliwafungia Real bao lao la pili dakika ya 61 kabla ya Asensio kukamilisha ushindi wao dakika ya 90 kwa bao lao la nne.
Juventus, waliokuwa wameanza vyema mechi hiyo wakikuwa wamekomboa bao la kwanza la Ronaldo dakika ya 27 kupitia Mario Mandzukic na kufanya mambo kuwa sare wakati wa mapumziko lakini kipindi cha pili mawimbi yaliwageuka.
Nguvu mpya wao Juan Cuadrado alipewa kadi ya pili ya manjano dakika ya 84, baada ya kukaa uwanjani dakika 18 pekee.
Gareth Bale aliingia kwenye mechi hiyo kama nguvu mpya, mara yake ya kwanza kuchezeshwa mechi ya ushindani tangu 23 Aprili.
Mechi hiyo iliyochezewa Cardiff ilikuwa ya 19 kwa klabu hizo mbili kukutana, mechi zote zikiwa katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya/Kombe la Ulaya.
Klabu hizo ndizo zilizokutana mara nyingi kabisa historia ya michuano hiyo, baada ya Bayern dhidi ya Real Madrid (24).

No comments