Rais Magufuli afanya ziara ya kushtukiza kiwanda cha viuatilifu vya malaria Kibaha
Rais
John Magufuli amefanya ziara ya kushtukiza katika kiwanda cha
kutengeneza dawa za kuulia vimelea vya mbu wanaosababisha malaria
kilichopo Kibaha, Pwani.
Magufuli
amevamia katika kiwanda hicho jana (Alhamisi) katika siku ya mwisho ya
ziara yake mkoani Pwani na kuzipa siku 10 halmashauri, manispaa na
majiji nchini kwenda kuchukua dawa hizo za kuua vijidudu vya malaria na
kuzipulizia katika maeneo yao yalipo makazi ya watu.
“Sasa
mimi nimeshatoa agizo dawa zilipiwe, sasa nione mkurugenzi ambaye
atashindwa kutekeleza agizo langu la kufata dawa hizo kwa kipindi
nilichotoa, nimesema natoa muda mpaka mwisho wa mwezi, "amesema Rais
Magufuli.
Kadhalika,
Rais ameiagiza Wizara ya Fedha kutoa Sh1.3 bilioni kwa ajili ya
kulipia lita 100 ya dawa hizo za kuua vimelea vya mbu zilizopo katika
kiwanda hicho.
Awali,
Kaimu Meneja wa kiwanda hicho, Samweli Mziray alimweleza Rais kuwa dawa
takribani lita 100 zipo tu kiwandani hapo baada ya wanunuzi wakuuu
ambao ni Halmashauri za Wilaya kushindwa kuzinunua kwa madai ya kukosa
fedha.
Kadhalika,
Mziray amefafanua zaidi na kumweleza Rais kuwa kushindikana kununuliwa
dawa hizo kwa wakati kunaweza kusababisha zikaharibika kwa sababu
zinatakiwa zisihifadhiwe zaidi ya miezi miwili tangu zinapotengenezwa.
Post a Comment