Picha: Harmonize amuonesha mzungu wake, ni mjamzito
Baada ya kuachana na mrembo wa filamu Tanzania Jacqueline Wolper, muimbaji wa wimbo Happy BirthDay kutoka WCB, Harmonize, ameonesha picha ya mpenzi wake mpya mzungu pamoja na kuthibitisha ni mjamzito.
Mpenzi mpya wa Harmonize
Muimbaji huyo ambaye alikuwa kimya kuzungumzia mahusiano yake mapya
na mzungu huyo licha ya kuzungumzwa na watu kwenye mitandao ya kijamii,
Jumapili hii ameonyesha vipimo vya Ultrasound vikionesha mpenzi wake
huyo mzungu ni mjamzito.“Mnh! nawaza huu mchanganyiko wa damu ya kimakonde na ya kizungu sijui itatuletea mwana gani… asa nikiona kakomwe hapo, kananistua
Hata hivyo muimbaji huyo hakuweka wazi ujauzito huo ni wa miezi mingapi.
Post a Comment