Shamsa Ford
Kupitia mtandao wa Instagram wa Shamsa ameandika, “Tujifunze
kusifiana tukiwa hai siyo mpaka mtu afe ndo umsifie, naomba nitumie
nafasi hii kukupongeza msanii mwenzangu una vitu vingi vikubwa ambavyo
wasanii wengi wa kike tunatakiwa kukuiga, la kwanza napenda bidii yako
ya kufanya kazi, wewe ni mwanamke mpambanaji sana, unajituma sana
kiukweli na wala hukati tamaa.

Jennifer Kyaka
“Pia ni mtu ambae hata ukipata mafanikio siyo mtu wa kujionesha na
wala huna mbwembwe. Lakini kubwa kuliko vyote napenda unavyoweka
mahusiano yako ya mapenzi private, sijawahi ona hata siku moja umempost
sijui boyfriend na hicho ndo kitu kizuri kwa mtoto wa kike,” aliongeza
Shamfa.

Jennifer Kyaka
“Mimi kwa upande wangu ningerudisha siku nyuma kipindi kile nipo
single nisingempost au kumuweka wazi mwanaume yoyote niliyekuwa naye
kipindi kile. Natamani mume wangu ndo angekuwa mwanaume wa kwanza kwa
watanzania kumjua, natamani wasanii wengi wa kike wangeiga mfano kwako.
Misingi uliyojiwekea kwenye maisha yako ni mizuri sana dada yangu, una
heshima na thamani kubwa sana. Hongera sana Jennifer Kyaka,” alifafanua
zaidi.
Post a Comment