Mwambusi Ataja Mchawi wa Yanga Baada ya Kutolewa Mapema Kwenye SportPesa Cup..!!!
Kocha msaidizi wa Klabu ya Yanga SC, Juma Mwambusi amefunguka na
kuitetea klabu yake baada ya kichapo cha goli 4-2 dhidi ya AFC Leopards
kutoka Kenya na kutupwa nje ya michuano ya SportPesa Super Cup kwa
kusema timu yake imekosa muda wa maandalizi.
Juma Mwambusi ambaye kwenye michuano ya Supersport Super Cup amechukua
nafasi ya Kocha mkuu Lwandamina aliyelikizo amesema Klabu ya Yanga
imetolewa kwa kukosa muda wa maandalizi kwani michuano hiyo haikuwa na
muda mrefu wa kuruhusu vilabu kujiandaa.
“Tumetolewa kweli michuano ilikuwa ni migumu kwetu hatukuwa na muda wa
kutosha wa maandalizi ya michuano hii muda ulikuwa mfupi sana, hii
imetuathiri sana kwenye michezo yetu yote miwili”Amesema Mwambusi mapema
baada ya mchezo kumalizika.
Klabu ya Yanga inakuwa timu ya nne kutolewa kwenye michuano hiyo yenye
msisimko wa aina yake inayodhaminiwa na kampuni ya Kubashiri ya
SportPesa, baada ya Simba,Singinda United na Jang’ombe Boys ya Zanzibar.

Post a Comment