Mtanzania Ahukumiwa Jela Kwa Kutupia Picha za Marehemu Facebook
Mwanaume
mmoja anayedaiwa kuwa ni Mtanzania amehukumiwa kifungo cha miezi mitatu
jela nchini Uingereza kwa kosa la kurusha katika ukurasa wake wa
Facebook, picha za mtu aliyefariki dunia kutokana na moto uliounguza
jengo la ghorofa la Mnara wa Grenfell lililopo nchini humo.
Pia, mtu huyo ametakiwa kulipa faini ya Sh579,880 kwa mwathirika wa tukio hilo.
Mtanzania
huyo, Omega Mwaikambo (43) alituma video na picha za mwili wa marehemu
uliokuwa kwenye begi na baadaye picha nyingine tano zikionyesha uso wa
marehemu huyo.
Gazeti
la mtandaoni la The Telegraph limeandika kuwa Mwaikambo amekiri makosa
ya kutuma mara mbili picha zisizopendeza kwa umma katika mitandao ya
kijamii mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Westminster jana.
Mwaikambo
ambaye anaishi hatua chache kutoka lilipo jengo la Grenfell akifanya
shughuli za upishi, alishuhudia jinsi jengo hilo lilivyoungua moto usiku
na alikuwa ni miongoni mwa wapishi waliowapikia chai wafanyakazi wa
zimamoto walipokuwa wakizima moto huo.
“Lakini
juzi Jumatano asubuhi alipoangalia miili hiyo nje ya nyumba yake
alichukua picha kwa kutumia simu yake aina ya iPad na kuzipakia kwenye
mtandao wake wa Facebook,” liliandika gazeti hilo.
Mwendesha
Mashtaka wa Polisi, Tom Little amesema; “Anaishi karibu zaidi na mnara
wa Grenfell, kama ambavyo mahakama inajua janga hilo lilitokea Juni 14.”
Akitoa
hukumu, Jaji wa mahakama hiyo, Tanweer Ikram amesema; “Dunia nzima
imeshtushwa na yaliyotokea hapa kutokana na janga la moto, ni hali ya
kutisha isiyostahimilika, wafu ni lazima waheshimiwe.”
Ameongeza;
“Ulichokifanya kupakia hizo picha kwenye Facebook ni dhahiri kuwa
hujaonyesha heshima kwa waathirika wa tukio hilo, kuonyesha uso wake
hadharani ni kosa kubwa na halielezeki.”
Post a Comment