Header Ads

Motra The Future afunguka baada ya media kadhaa kugoma kucheza nyimbo zake


Rapper Motra The Future amefunguka baada ya kudaiwa kuwa nyimbo zake hazichezwi kwenye baadhi ya vituo kwa kuwa yupo chini ya kituo fulani cha Radio
.
Motra amepinga madai hayo na amesema yeye support kubwa anayoipata ni kutoka kwa kundi la Weusi na wala hana menejimenti yoyote inayosimamia kazi zake.
“Mimi sina menejimenti yoyote ila ninapata support kutoka kwa mabrother Weusi. Na kuhusiana mimi ni msanii wa Clouds, hapana mimi siliafiki ila ni kwamba ninafanya kazi na watu wanajielewa, kwa hiyo mimi popote pale watu wanafanya kazi inayohusiana na kazi yangu lazima unikute,” rappe huyo ameiambia Metro FM ya Mwanza.
Kwa sasa Motra anafanya vizuri na wimbo wake ‘Sina Koloni’ ambao amemshirikisha G Nako.

No comments