Header Ads

Mnaoiponda Manchester United msikilizeni Pogba

Msimu uliopita maneno yalikuwa mengi yakielekezwa kwa Manchester United na mengi ya maneno hayo yalikuwa ya kuiponda klabu hiyo kongwe nchini Uingereza.
Wengine wanasema United haivutii, wengine wanasema wanatumia kiasi kikubwa cha pesa huku kiwango wanachoonesha uwanjani hakiendeni na pesa wanayotoa.
Paul Pogba naye ni mchezaji ambaye aliifanya United ipondwe sana kwani alisajiliwa kwa pesa nyingi sana lakini kiwango chake uwanjani kikawa cha kawaida sana.
Sasa wakati Paul Pogba akiwa mapumzikoni alizungumza na vyombo vya habari ambapo amesema anashangazwa sana na kauli za watu kuiponda United huku ina makombe matatu.
Pogba anasema anashangaa kuona timu yao ikipondwa kila mahala huku wana kombe la Carling Cup, Europa, ngao ya hisani huku wakiwa na tiketi ya kucheza Champions League.
“Tunaitwa timu mbovu (kicheko kikubwa sana),tunaitwa timu mbovu na tuna makombe matatu?hahaha kweli tunadaiwa hatujafanya hiki na kile lakini ninachojua timu mbovu tumebeba makombe matatu” alisema Pogba.
Kuhusu usajili wake mkubwa Paul Pogba amesema tangu anakuja katika klabu hiyo alikuwa anajua presha atakutana na presha katika klabu hiyo lakini hahitaji mumshauri.
“Kwanza ulikuwa msimu wangu wa kwanza hapa na nikicheza vizuri ninajua na nikicheza vibaya pia ninajua sasa sihitaji mtu aniambie kuhusu ninavyocheza kwani najua ninachokifanya” alimalizia Pogba.

No comments