Mambo mawili yanayompa furaha Beka Flavour nje ya Yamoto Band
Muimbaji huyo ambaye anatamba na wimbo ‘Libebe’ amekiambia kipindi cha Dj Show cha Radio One, kuwa mambo anayofurahia ni kuimba wimbo mzima pekee yake na uhuru wa kujiamulia mambo binafsi katika muziki.
“Vitu vingi vilikuwa vinanizuia, kwanza nilikuwa si-enjoy kwa sababu nilikuwa naimba verse fupi, mwenywe nilikuwa natamani niimbe verse ndefu lakini wenzio wataimba wapi, hicho ni kitu cha kwanza kilikuwa kinanibana,” amesema Beka Flavour.
Ameongeza “Kuna vitu vingi vimefunguka kupitia mimi mwenyewe, kwanza ilikuwa mtu akinihitaji ni lazima apitie kwa mtu mwingine na mwingine, au kuna kitu kingine ambacho mimi napenda kufanya zaidi ila uongozi unakuta unabana lakini sasa hivi vile navyopenda kuvifanya nafanya na uongozi upo.”
Post a Comment