Lava Lava-Sio kila msanii wa WCB anaimba kama Diamond
Msanii mpya wa muziki kutoka WCB, Lava Lava amedai sio kweli kwamba wasanii wengi wa label hiyo wanaimba kama rais wa label hiyo, Diamond Platnumz.
Harmonize na Rayvanny ni kati ya wasanii wa label hiyo ambao wamekuwa wakifanishwa katika uimbaji na Diamond.
Akiongea na Bongo5 wiki hii, Lava Lava amewataka mashabiki wa muziki kuwasikiliza vizuri waimbaji hao huku akidai kila msanii wa label hiyo ana aina yake ya uimbaji.
“Naona watu wanazungumza lakini watu wawe na masikio ya kusikiliza kitu,” alisema Lava Lava. “Sio watu wote wanaweza kufanana ya Diamond japokuwa kuna vitu tunaweza kufanana kwa sababu ni watu ambao tunakaa pamoja kwa muda mrefu. Pia watu wakiwa wanaishi muda mrefu pamoja huwa wanafanana, kwa hiyo kuna muda mkikaa pamoja kuna vitu mnaanza kushare lakini ukichunguza ndani yake kila mtu ana kitu chake,”
Post a Comment