Header Ads

Hector Bellerin amuweka Wenger njia panda: Safari ya kurejea Barcelona yaiva

Image result for hector bellerin and wenger
Beki wa pembeni wa klabu ya Arsenal, Hector Bellerin huenda akaihama klabu hiyo na kurejea jijini Barcelona Hispania kujiunga na Klabu yake ya utotoni ya FC Barcelona katika kipindi hiki cha usajili wa majira ya kiangazi.
Bellerin (22) ameonesha nia ya kuondoka Arsenal, kufuatia kauli yake aliyoitoa wakati akihojiwa na gazeti la Mundo Deportivo jana jumanne huku kauli hiyo ikionekana kumuumiza zaidi mzee Wenger ambaye bado anahitaji uwepo wake.
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger na Bellerin
Bellerin ambae yupo Hispania kwa ajili ya mechi za kimataifa za FIFA wakati akihojiwa na Gazeti la Mundo Deportivo jana alisema “Nipo hapa kwa ajili ya kuitumikia Arsenal, ninaipenda na kuithamini, lakini likitokea la kutokea nitaondoka na kwenda popote pale ninapohitajika ,”
Kuhusu kuwindwa na Klabu ya Barcelona, Bellerin amesema “Ndiyo najisikia furaha kusikia klabu kubwa kama Barca wamevutiwa na uchezaji wangu nitafurahiikitokea“.
Mhispania huyo alishawahi kuitumikia klabu ya Barcelona akiwa mdogo hata kabla ya kwenda Arsenal na ni moja ya wachezaji ambao mzee Wenger ameshatangaza kuwahitaji kwenye kikosi chake msimu ujao mapema baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo mwezi uliopita.

No comments