Hakuna muasisi wa hip hop asiyekuwa na nyimbo ya mapenzi – Stamina
“Mapokezi ya kufanya ngoma ya mapenzi yamekuwa makubwa sana, ngoma imekuwa cheche ndani ya siku moja. Lakini siyo kama ndio tutaacha kuimba nyimbo za harakati, mapenzi yenyewe ni harakati watu wanasahau kuwa mapenzi ni moja kati ya sehemu ya maisha ya jamii,” Stamina amekiambia kipindi cha Dj Show cha Radio One.
“Watu wamekuwa wakichukulia mtu wa Hip Hop akiimba nyimbo ya mapenzi ndio kashabadilisha harakati, hakuna kuna vitu vingi vya kuongelea katika jamii moja wapo ni mapenzi. Hata waasisi wa zamani wa Hip Hop wakina Tupac, kina B.I.G kina nani wote wana nyimbo za mapenzi, hakuna muasisi wa Hip Hop asiyekuwa na nyimbo ya mapenzi,” ameongeza.
Post a Comment