Diamond ili Uwe na Sifa ya Ziada ya Kujiunga na WCB,Ni lazima Utoke Katika Familia ya Kimasikini Kabisa..!!!

Rais wa lebo ya WCB, Diamond Platnumz ametaja sifa za kujiunga na lebo
hiyo. Msanii huyo amesema ni lazima uwe umetoka katika maisha ya chini
kabisa, yaani familia isiyojimudu kiuchumi.
Diamond amesema hawawezi kuchukua watu wanaotokea familia zinazojimudu
kiuchumi [tajiri] kwa sababu ni vigumu kwa wao kupambana kwa kuwa kila
kitu wanacho.
“Sifa ya kwanza WCB ni mtu aliyetoka katika hali ngumu, maisha magumu
kwa sababu sisi tunajitahidi kujiajiri mwenyewe kwa wenyewe. Japo kuwa
muziki wetu haujawa na riziki lakini angalau kidogo hichi tule wote,”
amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM.
“Tunaamini watu kutoka mtaani wanakuwa na talent ya kweli, wanakuwa na
njaa ya kujituma na nidhamu kwa sababu wanaogopa wasije wakarudi tena
katika mtaa. Lakini mtoto wa kitajiri mimi sikudanganyi wanakuwa hawana
nidhamu kwa sababu wanajua sisi tuna hela, kwa hiyo yeye haogopi au
kufanya kazi kwa bidii,” ameongeza.
Diamond amesisitiza ni mara kumi wakatumia nafasi walionayo kuwasadia
wale walio mtaani kwa sababu wapo wengi na wanahitaji kushikwa mkono ili
kesho na kesho kutwa wakazisaidie familia zao.
Post a Comment