CHADEMA Watoa Ushauri kwa Rais Magufuli Sakata la Madini......Wasema Wapo Tayari Kushirikiana Nae
Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimedai kuwa kipo tayari
kumuongoza Rais John Magufuli katika kulinda rasilimali za Taifa ikiwemo
madini, huku kikiwataka wananchi kuishauri serikali kuchukua hatua
kwanza badala ya kuipongeza kuhusu sakata la Makinikia.
Wakati
akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Katibu
Mkuu Chadema, Dkt. Vincent Mashinji amedai kuwa, hatua anazochukua Rais
Magufuli kuhusu Makinikia ziko kinyume na Ilani ya CCM ambapo katika
ukurasa wake wa 26-28 haikuzungumzia kurekebisha sheria na mikataba ya
madini, na kwamba ilani ya Chadema kwenye ukurasa wake wa 57-59
inaonyesha namna ya kuiongoza vizuri sekta ya madini.
“Rais
hatafaulu vita hii kama serikali yake itaendelea kutubagua au
kutosikiliza sauti ya upande wa pili. Pia watu wasiwe wa kutoa pongezi
kabla kazi haijaisha. Kama tunatakiwa kulipwa trilioni mia, wajue kwamba
za kwetu ni asilimia 4 tu, na hii ndiyo matokeo ya mikataba
tuliyoilaani kila siku. mrabaha wetu ni asilimia 4 huku wawekezaji
kwenye pesa hizo za kwao ni 96%,” amesema.
Hata
hivyo, Dkt. Mashinji ametaja hatua kadhaa ambazo amedai kuwa kama Rais
Magufuli atazichukua, zitamuwezesha kushinda vita aliyoianzisha ikiwemo,
kuleta katiba mpya, kurudisha ‘Bunge Live’ ili watanzania wawaone
wabunge ambao ni mawakala wa uporaji rasilimali za nchi, ili wawahuku
katika chaguzi zijazo.
“Kama
anataka kulifanikisha hili kwa uwazi arudishe bunge live, arudishe
mikutano ya hadhara sisi tusimame tuwaambie watanzia, tuwataje mafisadi
wako wapi ili twende kupambana nao,” amesema.
Hatua
nyingine alizotaja, ni kuzitoa hadharani ripoti zote mbili za
makinikia, kuweka wazi mikataba ya siri iliyopitishwa na Bunge,
kuwachukulia hatua waliohusika na upotevu wa rasilimali, pamoja na
kuyafanyia kazi maoni ya wapinzani.
Post a Comment