Header Ads

Brand yangu inaruhusu kutoa wimbo mmoja kwa mwaka – Kala


Msanii wa muziki wa hip Hop, Kala Jeremiah amefunguka kwa kudai kuwa yeye ni mmoja kati ya wasanii wachache Tanzania ambao wanaweza kuachia wimbo mmoja kwa mwaka.

Rapa huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Wanandoto’ ameiambia Bongo5 kuwa nyimbo zake huwa ana ziandaa ili ziweze kufanya vizuri kwa muda mrefu.
“Mimi kwenye muziki wangu wimbo mmoja unatosha kwa mwaka kwa sababu natoa wimbo wenye nguvu kubwa, natoa wimbo ambao una meseji kubwa pia natoa wimbo ambao utasikiliza na watu wengi wa rika zote,” alisema Kala.
Kala amedai wasanii wengi wanatoa nyimbo kila mara ili waendelee kubaki kwenye masikio ya watu.
Katika hatua nyingine rapa huyo amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa mkao wa kula kwaajili ya ujio wa kazi mpya.

No comments