Bajeti Kuu ya Serikali 2017/18..Pato la Mtanzania Laongezeka kwa Asilimia 11...!!!
Pato la kila mtanzania kwa mwaka 2016 limeongezeka kwa asilimia 11
kutoka shillingi 1,918,897 kwa mwaka 2015 mpaka kufikia shilling
2,131,299 kwa mwaka 2016.
Takwimu hizi zimebainishwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Philip
Mpango wakati akiwasilisha Bungeni Mjini Dodoma Taarifa ya Hali ya
Uchumi ya mwaka 2016 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa mwaka
2017/2018.
Akifafanua kuhusu ongezeko hilo Mhe. Dkt Philip Mpango amesema kuwa Pato
la Taifa kwa mwaka 2016 lilifikia Shillingi million 103,744,606 kwa bei
za mwaka husika na kiasi hiki kiligawanywa kwa idadi ya watu 48,676,698
walipo Tanzania Bara na kufanya wastani wa Pato la kila mtanzania
kufikia kiasi cha Shillingi 2,131,299.
Ameeleza kuwa kwa thamani ya Dola za Marekani, wastani wa pato la Kila
mtu liliongezeka kutoka Dola 967.5 mwaka 2015 hadi Dola 979.1 kwa mwaka
2016 ikionesha kuwa Tanzania inaelekea kwenye kundi la Uchumi wa kati.
“Serikali inaendelea kutatua changamoto mbalimbali ili tuweze kufikia
Uchumi wa Kati kwa kuongeza fursa mbalimbali za uzalishaji nchini,”
alisistiza Mhe. Dkt Mpango.
Mhe. Dkt. Phili Mpango ameongeza kuwa Serikali imejipanga kuboresha
shughuli za uzalishaji wa tija katika Sekta zinazoajiri hususan katika
Sekta ya Kilimo cha mazao,Ufugaji na Uvuvi.

Post a Comment