Baada ya Kimya Kirefu..Makonda Aibuka na Haya Makubwa Kuhusu Jeshi la Polisi...!!!
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema jeshi la Polisi
katika Mkoa huo linatakiwa kuwa la mfano wa kuigwa katika kukabiliana na
kila wimbi la uhalifu, ili wananchi waishi kwa amani kutokana na
umuhimu wa biashara.
Makonda ameyasema hayo wakati wa kupeleka magari 26 ya polisi kwenye
ukarabati katika gereji iliyoko maeneo ya Utalii mkoani Kilimanjaro, kwa
ajili ya matengenzo pamoja na ufungaji wa Kamera katika magari hayo
alipokuwa anazungumza na jeshi la polisi leo Osterbay jijini Dar es
Salaam.
Amesema katika kukabiliana na rushwa na jeshi hilo, watafunga kamera
katika kila kituo ndani ya jiji la Dar es Salaam, ambapo OCD , kanda
maalumu, pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi wataweza kuona kile ambacho
kinafanyika.
Makonda amesema jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es Salaam linatakiwa kuwa la
kisasa zaidi katika kukabiliana na uhalifu wa kila namna ikiwa ni
pamoja na kuwa na vifaa vya kisasa.
Amesema katika maboresho hayo wataweka Kompyuta kila kituo ili kuachana
na kuandika maelezo katika karatasi na mtu yeyote, baada ya kuwekwa
kompyuta hizo asikubali kuandikiwa maelezo katika karatasi.
Aidha amesema kuna baiskeli ziko njiani ambazo zitagawiwa kwa polisi
ikiwa ni sehemu ya kukabiliana na uhalifu katika mazingira ambayo kifaa
hicho kinaweza kupita.
Nae Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lucas Mkondya
amesema Jeshi la Polisi kanda maalumu inakabiliwa na changamoto ya
magari pamoja na mafuta na kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi katika
kukabiliana na wahalifu wa kila namna .
Amesema kuwa kutokana maboresho hayo yataweza kubadilisha hata takwimu
zilizo katika kipindi hiki zisirudie kutokana na maboresho hayo.
Post a Comment