Alexis Sanchez chaguo la kwanza la usajili- Manchester City
Mchezaji wa klabu ya Arsenal ya ligi kuu nchini Uingereza, Alexis Sanchez ameendelea kuwa chaguo namba moja kati ya wachezaji wanaohitajika ndani ya kikosi cha Manchester City licha ya wenyeji hao wa Etihad kushindwa kuliweka wazi mbele ya Arsenal.
Mchezaji wa klabu ya Arsenal, Alexis Sanchez akiwa na kocha wa Man City Pep Guardiola
The Gunners mpaka sasa haijampa mkataba mpya mchezaji huyo wa kimataifa wa Chile mwenye umri wa miaka 28 ambaye ameshinda jumla ya magoli 30 katika msimu uliomalizika wa mwaka 2016/17.
Sanchez, amesema mustakabali wa hatima ya maisha yake ya baadae upo mikononi mwa wakala wake na hivyo yeye yupo katika majukumu ya timu ya taifa.
Klabu za City pamoja na Bayern Munich zimeonyesha nia ya kuhitaji huduma ya mshambuliaji huyo ambaye yupo katika majukumu na timu yake ya Chile.
Wachezaji wa klabu ya Arsenal, Mesut Ozil(kushoto) pamoja na Alexis Sanchez (kulia)
Meneja, Arsene Wenger amesaini mkataba wa miaka miwli ya kuendelea kukitumikia kikosi hiko baada ya kutwaa taji la FA Cup dhidi ya Chelsea,na hivyo kusisitiza wachezaji Sanchez pamoja na Mesut Ozil kamwe hawato uzwa.
Post a Comment