Header Ads

Watu 11 wauawa na tufani mji mkuu wa Urusi, Moscow

Moscow. 29 Mei 2017Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionGari likiwa limeinuliwa na mizizi ya mti ulioanguka baada ya tufani kukumba Moscow
Watu zaidi ya 11 wamefariki baada ya tufani kukumba mji mkuu wa Urusi, Moscow, maafisa wa afya wanasema.
Upepo huo mkali uling'oa mamia ya miti, na zaidi ya watu 50 walitafuta matibabu.
Taarifa zinasema nyaya za umeme pia ziliharibiwa baada ya mvua kubwa iliyoandamana na upepo mkali kukumba mji wa Moscow.
Upepo mkali uliovuma kwa kasi ya hadi 110 km/h (70 mph) ni jambo ambalo watabiri wa hali ya hewa walisema ni nadra sana kutokea mjini humo.
Wanasema upepo huo uliathiri majengo.
Iwapo idadi hiyo ya waliofariki itathibitishwa, basi itakuwa idadi kubwa zaidi ya watu kuuawa na tufani mjini humo katika kipindi cha zaidi ya miaka 100.
Kremlin SenateHaki miliki ya pichaJOHN WILKINSON
Image captionPaa la jumba la Seneti la Kremlin liliharibiwa na upepo huo
Moscow, Russia, 29 May 201Haki miliki ya pichaEPA
Image captionWengi waliuawa an miti iliyong'oka na kuanguka
Mti ulioanguka MoscowHaki miliki ya pichaEPA
Meya wa Moscow Sergei Sobyanin alituma salamu za rambirambi kwa jamaa na marafiki wa waliofariki.
Maafisa wa baraza la mji wanafanya juhudi kuondoa miti iliyoanguka na kuziba barabara.
Rais wa Urusi Vladimir Putin alikuwa Versailles, karibu na Paris siku ya Jumatatu akifanya mashauriano na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.

No comments